Zaburi 119

Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

Psalm 119:115 (UKJV) Depart from me, all of you evildoers: for I will keep the commandments of my God.

113Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.

114Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.

115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

116Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.

117Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.