128na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu.
129Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii.
130Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
131Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.
132Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.