161Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
162Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.
163Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, lakini napenda sheria yako.
164Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki.
165Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.