171Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
172Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.
173Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako.
174Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.
175Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze.