30Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
31Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe.
32Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.
33Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.
34Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.