28Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako.
29Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.
30Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
31Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe.
32Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.