48Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako.
49Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.
50Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
51Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako.
52Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji.