50Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
51Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako.
52Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji.
53Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.
54Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi.