58Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.
59Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.
60Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.
61Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako.
62Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.