60Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.
61Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako.
62Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.
63Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, kwa wote wanaofuata mausia yako.
64Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.