Zaburi 119

Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.

Psalm 119:68 (UKJV) You are good, and do good; teach me your statutes.

66Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.

67Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

68Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.

69Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

70Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.