Zaburi 119

Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.

Psalm 119:66 (UKJV) Teach me good judgment and knowledge: for I have believed your commandments.

64Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.

65Mtendee wema mtumishi wako Ee Bwana, sawasawa na neno lako.

66Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.

67Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

68Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.