19Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!
20Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako.
21Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?
22Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu.
23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu.