10Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
11Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,
12ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.