13Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote;
14kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani:
15yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
16Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake; hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake.
17Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.