12Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.
13Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote;
14kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani:
15yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
16Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake; hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake.