5Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma.
6Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
7Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye chungu; vilindi vya bahari ameviweka katika ghala.
8Dunia yote na imwogope Bwana, watu wote wa dunia wamche.
9Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, aliamuru na ikasimama imara.