Zaburi 38

Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.

Psalm 38:15 (UKJV) For in you, O LORD, do I hope: you will hear, O Lord my God.

13Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake,

14nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu.

15Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.

16Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”

17Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.