15Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.
16Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”
17Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote.
18Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu.
19Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, wale wanaonichukia bila sababu ni wengi.