8Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, au sadaka zako za kuteketezwa, ambazo daima ziko mbele zangu.
9Sina haja ya fahali wa banda lako, au mbuzi wa zizi lako.
10Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu.
11Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu.
12Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, kwa maana ulimwengu ni wangu, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.