1Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua.
2Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza.
3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.
4Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: