3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.
4Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake:
5“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, waliofanya agano nami kwa dhabihu.”
6Nazo mbingu zinatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu.
7“Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu.