14Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.
15Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
16Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa.
17Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.
18Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.