Zaburi 51

Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.

Psalm 51:17 (UKJV) The sacrifices of God are a broken spirit: a broken and a contrite heart, O God, you will not despise.

15Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.

16Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa.

17Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.

18Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.

19Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.