Zaburi 7

Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.

Psalm 7:15 (UKJV) He made a pit, and dug it, and is fallen into the ditch which he made.

13Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.

14Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.

15Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.

16Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani.

17Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.