11Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.
12Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.
14Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
15Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.