3Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu,
4au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu,
5basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini.
6Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.
7Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu.