1Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe.
2Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe.
3Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
4Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.