1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi.
2Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.
3Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu.
4Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu.
5Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.