Zaburi 73

Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

Psalm 73:5 (UKJV) They are not in trouble as other men; neither are they plagued like other men.

3Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

4Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu.

5Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

6Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri.

7Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.