1Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli.
2Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni.
3Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita.
4Wewe unangʼaa kwa mwanga, mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.