Zaburi 78

yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia.

Psalm 78:3 (UKJV) Which we have heard and known, and our fathers have told us.

1Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu.

2Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:

3yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia.

4Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

5Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.