33Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho.
34Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku.
35Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.
36Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao,
37mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.