36Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao,
37mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote.
39Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.
40Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani!