41Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
42Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,
43siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani.
44Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.
45Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu.