43siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani.
44Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.
45Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu.
46Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige.
47Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.