45Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu.
46Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige.
47Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.
48Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.
49Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.