46Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige.
47Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.
48Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.
49Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.
50Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.