51Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.
52Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.
53Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao.
54Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.
55Aliyafukuza mataifa mbele yao, na kuwagawia nchi zao kama urithi, aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.