49Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.
50Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.
51Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.
52Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.
53Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao.