Zaburi 80

mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe.

Psalm 80:2 (UKJV) Before Ephraim and Benjamin and Manasseh stir up your strength, and come and save us.

1Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; wewe uketiye katika kiti cha enzi katikati ya makerubi, angaza

2mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe.

3Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa.

4Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi dhidi ya maombi ya watu wako?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.