3Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa.
4Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi dhidi ya maombi ya watu wako?
5Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
6Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki.
7Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa.