5Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
6Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki.
7Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa.
8Ulileta mzabibu kutoka Misri, ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.