1Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu.