Zaburi 86

Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.

Psalm 86:7 (UKJV) In the day of my trouble I will call upon you: for you will answer me.

5Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.

6Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie.

7Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.

8Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.

9Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.