3Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu.
5Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie.
7Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.