Zaburi 89

Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

Psalm 89:2 (UKJV) For I have said, Mercy shall be built up for ever: your faithfulness shall you establish in the very heavens.

1Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.

2Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

3Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi,

4‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.