34Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
35Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi:
36kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
37kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”
38Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.