16Basi Naomi akamchukua yule mtoto, akampakata na akawa mlezi wake.
17Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, “Naomi ana mtoto wa kiume.” Wakamwita jina lake Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
18Hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni,
19Hesroni akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu,
20Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,