29Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.
30Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
31Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
32Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
33Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.